fes.de
  • News
  • Trade Unions

Kazi the Podcast E11: Negotiating Fairness: The Power and Practice of Collective Bargaining

Collective bargaining gives workers a stronger voice in negotiating fair working conditions, while helping employers and employees build productive workplaces through dialogue, cooperation, and shared responsibility

Close-up of a handshake between two professionals in an office environment
Creator: Pavel Danilyuk/Pexels

Kazi the Podcast Toleo la 11: Nguvu ya Majadiliano ya Pamoja na Mikataba ya Hali Bora

Majadiliano ya pamoja yanawapa wafanyakazi sauti yenye nguvu zaidi katika kujadili mazingira ya kazi yaliyo ya haki, huku yakiwasaidia waajiri na waajiriwa kuongeza tija katika maeneo ya kazi kupitia mazungumzo, ushirikiano, na uwajibikaji wa pamoja.

Wafanyakazi wengi nchini Tanzania wanaendelea kukabiliana na changamoto kama vile mishahara midogo, mazingira duni ya kazi, kucheleweshewa mishahara, kutokuwa na uhakika wa ajira, na fursa chache za kushiriki katika kufanya maamuzi mahali pa kazi. Changamoto hizi zinaweza kuwa ngumu zaidi kwa vijana wanaoingia kwenye soko la ajira, wafanyakazi wenye mikataba ya muda mfupi, na wale walioajiriwa katika sekta isiyo rasmi. Ingawa sheria zinatoa taratibu za kulinda haki za wafanyakazi, waajiriwa wengi bado wanapata ugumu wa kuwasilisha kero zao na kujadiliana ili kupata mazingira bora ya kazi.

Masuala haya yalikuwa msingi wa Toleo la 11 la Kazi the Podcast. Toleo hili linawashirikisha Bw. Innocent John, Mkurugenzi wa Uchumi, Utafiti na Mipango kutoka Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), na Bi. Nice Amon Mwansasu, Mratibu kutoka Chama cha Wafanyakazi wa Mawasiliano na Uchukuzi Tanzania (COTWU-T). Wanajadili umuhimu wa majadiliano ya pamoja, uwakilishi wa wafanyakazi, na ushirikiano kati ya waajiri na wafanyakazi katika kuhamasisha mazingira ya haki na kazi yenye staha nchini Tanzania.

Nguvu ya Uwakilishi wa Pamoja

Majadiliano ya pamoja yanawapa wafanyakazi fursa ya kuungana kupitia vyama vyao vya wafanyakazi ili kujadiliana na waajiri kuhusu mambo yanayogusa mazingira yao ya kazi na maslahi yao. Badala ya kila mfanyakazi kumfuata mwajiri peke yake, wafanyakazi wanaweza kuteua wawakilishi wa kuwasilisha kero zao za pamoja na kujadiliana kwa niaba yao ili kupata maboresho.

Akitumia sekta ya madini kama mfano, Innocent John anaeleza kwa nini uwakilishi wa pamoja ni muhimu. Kwa mfano, wafanyakazi katika sekta hiyo wanaweza kutumia chama chao cha wafanyakazi, kama vile Chama cha Wafanyakazi wa Migodi, Nishati na Ujenzi (TAMICO), kuunganisha kero zao na kujadiliana na waajiri kupitia mwakilishi.

"Wafanyakazi na waajiri wanategemeana. Ili kuongeza tija mahali pa kazi, lazima kuwepo na mifumo thabiti inayowawezesha waajiri kuelewa changamoto za wafanyakazi, huku wafanyakazi nao wakielewa kile ambacho waajiri wanakitarajia kutoka kwao," anaeleza.

Mapatano ya Pamoja na Maboresho ya Mazingira ya Wafanyakazi

Tofauti na haki zinazotolewa chini ya sheria na kanuni za kazi, majadiliano ya pamoja yanaweza kutengeneza fursa za kuboresha mazingira ya wafanyakazi kupitia mazungumzo kati ya waajiri na wawakilishi wa wafanyakazi.

Nice Amon Mwansasu anaeleza kuwa mikataba inayotokana na majadiliano ya pamoja ni muhimu kwa sababu inagusa moja kwa moja maslahi na mazingira ya kazi ya wafanyakazi. Hata hivyo, kufikia maboresho hayo kunahitaji uwakilishi thabiti kutoka kwa vyama vya wafanyakazi ambavyo vinaweza kujadiliana na waajiri kwa niaba ya wanachama wao.

Mapatano ya pamoja hayaishii tu kwenye kutatua migogoro; yanaweza pia kuwa mfumo wa wafanyakazi kudai maslahi bora, mazingira yaliyoboreshwa, na ulinzi thabiti zaidi wa haki zao.

Mazungumzo, Ushirikiano, na Tija Mahali pa Kazi

Wakati mwingine majadiliano yanaweza kuchukuliwa kama ugomvi au msuguano kati ya wafanyakazi na waajiri. Hata hivyo, majadiliano hayo yanaweza kutoa fursa ya mazungumzo, ushirikiano, na kuelewana.

Kwa vijana wanaoingia kwenye soko la ajira, kuelewa mchango wa vyama vya wafanyakazi na majadiliano ya pamoja ni jambo la msingi sana. Inawasaidia kutambua thamani ya uwakilishi wa wafanyakazi na mifumo iliyopo ya kutatua changamoto zinazohusu mishahara, stahiki, mazingira ya kazi, na utendaji wa haki.

Kujenga Maeneo ya Kazi Yenye Haki na Ujumuishi

Majadiliano haya yanatilia mkazo umuhimu wa ushirikiano kati ya wafanyakazi, waajiri, vyama vya wafanyakazi, na serikali katika kuhamasisha kazi yenye staha nchini Tanzania. Kuongeza uelewa kuhusu haki za wafanyakazi, kuboresha uwakilishi, na kuweka mianya thabiti ya mazungumzo mahali pa kazi ni hatua muhimu kuelekea maeneo ya kazi yenye haki na tija zaidi.

Ujumbe mkuu wa Toleo hili la 11 ni kwamba majadiliano ya pamoja si tu kuhusu kudai mazingira bora au kutatua migogoro. Ni mchakato wa kutengeneza uelewa wa pamoja kati ya wafanyakazi na waajiri, kujadiliana maboresho, na kujenga mahusiano ya kazi yenye manufaa kwa wote.

Wakati Tanzania ikiendelea kuhamasisha kazi yenye staha na ukuaji wa uchumi unaoshirikisha wote, majadiliano ya pamoja yanabaki kuwa mfumo muhimu wa kuhakikisha wafanyakazi wanakuwa na sauti katika maamuzi yanayogusa maisha na riziki zao.

Sikiliza toleo hili kamili la Kazi the Podcast kupitia Spotify, Apple Podcasts, YouTube Music, SoundCloud, na tovuti ya FES Tanzania.

Many workers in Tanzania continue to face challenges such as low wages, poor working conditions, delayed salaries, job insecurity, and limited opportunities to participate in workplace decision-making. These challenges can be particularly difficult for young people entering the labour market, contract workers, and those employed in the informal sector. Although labour laws and institutions provide mechanisms for protecting workers’ rights, many employees still face difficulties in raising concerns and negotiating for better working conditions.

These issues were at the center of Episode 11 of Kazi the Podcast, titled Negotiating Fairness: The Power and Practice of Collective Bargaining. The episode features Innocent John, Director of Economics, Research and Planning at the Trade Union Congress of Tanzania (TUCTA), and Nice Amon Mwansasu, Coordinator at the Communications and Transport Workers Union of Tanzania (COTWU-T). They discuss the importance of collective bargaining, worker representation, and cooperation between employers and employees in promoting fair working conditions and decent work in Tanzania.

The Power of Collective Representation

Collective bargaining allows workers to come together through their trade unions to negotiate with employers on matters affecting their working conditions and interests. Rather than approaching employers individually, workers can appoint representatives to communicate their shared concerns and negotiate for improvements on their behalf.

Using the mining sector as an example, Innocent John explains why collective representation is important. Workers in the sector, for instance, can use their trade union, such as the Tanzania Mines, Energy, Construction and Allied Workers’ Union (TAMICO), to bring their concerns together and negotiate with employers through a representative.

“Workers and employers depend on each other. To improve productivity in the workplace, there must be effective systems that enable employers to understand workers’ challenges, while workers must also understand what employers need from them,” he explains.

Collective Agreements and Improving Workers’ Conditions

Beyond the rights provided for under labour laws and regulations, collective agreements can create opportunities to improve workers’ conditions through negotiations between employers and recognised worker representatives.

Nice Amon Mwansasu explaines that collective agreements are important because they directly affect workers’ welfare and working conditions. However, achieving improvements requires effective representation by trade unions, which can negotiate with employers on behalf of their members.

Her contribution underlines that collective bargaining is not limited to resolving disputes. It can also provide a mechanism for workers to seek better benefits, improved conditions, and stronger protection of their rights.

Dialogue, Cooperation, and Workplace Productivity

Collective bargaining is sometimes perceived as a confrontation between workers and employers. However, the discussion highlighted that it can instead provide a structured platform for dialogue, cooperation, and mutual understanding.

For young people entering the labour market, understanding the role of trade unions and collective bargaining is particularly important. It can help them recognise the value of worker representation and the mechanisms available for addressing concerns about wages, benefits, working conditions, and fair treatment.

Building Fairer and More Inclusive Workplaces

The discussion highlights the importance of cooperation among workers, employers, trade unions, and the government in promoting decent work in Tanzania. Strengthening awareness of labour rights, improving worker representation, and establishing effective channels for workplace dialogue are important steps towards fairer and more productive workplaces.

The central message of Episode 11 is that collective bargaining is not simply about demanding better conditions or resolving disputes. It is about creating a process through which workers and employers can understand one another, negotiate improvements, and establish mutually beneficial working relationships.

As Tanzania continues to pursue decent work and inclusive economic growth, collective bargaining remains an important mechanism for ensuring that workers have a voice in decisions affecting their lives and livelihoods.

Listen to the full episode of Kazi the Podcast on Spotify, Apple Podcasts, YouTube Music, SoundCloud, and the FES Tanzania website.